EKARISTI TAKATIFU
Uwepo wa YESU wa Ekaristi huanza dakika ya mageuzo na hudumu muda wote ambao maumbo ya Ekaristi yapo. KRISTO ni wote kabisa katika kila umbo, na ni wote kabisa katika kila sehemu yao, kwa jinsi hii kwamba kumega mkate hakumgawanyi KRISTO. (Paulo VI) Hata kichembe kidogo namna gani KRISTO ni wote kabisa. “Basi akawaambia, “Amin, Amin,nawaambieni: Msipokulamwili wake mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; name nitamfufu siku ya mwisho.” (Yoh. 6:53-54)
Kuna mambo ambayo yanashughulikiwa tu na Baba Mtakatifu kwa namna ya pekee=Kutupa au kuchukua au kuwanayo Ekaristi Takatifu kwa nia ovu.
KUPOKEA EKARISTI TAKATIFU MKONONI NI KUSIHIMIZWE.
Cha msingi ni kwamba: Wakatoliki wanaokomunika waungame kwanza dhambi zao ndipo wamaribie YESU wa Ekaristi (Mfalme wa wafalme, BWANA wa mabwana, MUNGU mwenye enzi kuu amabye huwezi kumfananisha na yeyote awaye yule) na wampokee wakiwa wamepiga magoti mdomoni. (Zamani) Wasikufuru kwa kumpokea YESU wa Ekaristi wakiwa katika hali ya dhambi. Kupokea kwa kustahili na kupata mafaa ya Komunyo, kunahitaji maandalizi ya dhati kwa upande wa mkonunikaji:
i. anapaswa kutokuwa na dhambi ya mauti yoyote,
ii. anapaswa kuwa na huzuni kwa dhambi ndogo zote na kujitahidi kuzishinda
iii. anapaswa kufunga chakula au vimiminika (isipokuwa maji) angalau saa moja kabla ya kupokea,
iv. anapaswa kushiriki kikamilifu katika Ekaristi ambamo anapokea.
· Papa Paul II, Nov. 1980, Ujerumani. “Kuna barua ya kitumeinayoruhusu kupokea Ekaristi Takatifu kwenye mkono. Lakini nawaambieni sipendekei zoezi hilo wala si shauri.”
· Mama Teresa wa Calcuta, India, alipohojiwa mwaka 1989 akiwa New York kuhusu kile anachofikiri kuwa ni jambo baya zaidi katika dunia ya sasa, yeye alijibu bila kusita na kusema; “Popote ninapokwenda dunia nzima, kitu abacho kinanifanya niwe na huzuni sana ni kuwaona watu wakipokea Ekaristi Takatifu kwa mikono.” Katika shirika lake masita wake wote walikuwa wakipokea Ekaristi Takatifu mdopmoni.
· Askofu Juan Rudolf aliwahi kusema; “Kwa kupokea Ekaristi Takatifu mkononi, muujiza unatakiwa wakati wa kugawa Ekaristi ili kuepuka vipande vya hostia visianguke au kubaki mkononi mwa mpokeaji. “
Kuthibitisha hili ni barua ya toba kwa Baba Mtakatifu Yohane Paulo VI aliyoiandika Charles Andre akiungama kwa kutupa au kusababisha kutupwa kwa takribani Komunyo 60,000 tangu mwaka 1980 ahdi 1991 na kusababisha hostia hizi kuendelea kukaknyagwa. Kwa vile alifanya vile bila kujali. Hata wapokeaji nao hawakujali.
Katika uchunguzi wake, aligundua kuwa wastani wa vipande 3.68 vya komunyo hubakia kwa mpokeaji. Hii ni kwa vile alifanya jaribio kwa kutumia hostia zilizotoka kwenye viwanda vinavyotengeneza hostia kwa kiwango cha hali ya juu sana, (Ubaora).
Alifanya uchunguzi akiwa na mtoto wake. Walinunua hostia zilizokuwa na ubora wa hali ya juu ambazo kingo zake zilikuwa imara. Waliosha mikono yao vizuri sana na kuikausha vema. Kisha, alimpokelesha mtoto wake mkonopni naye akachukua kwa vidole akala. Kisha walihesabu vipande vilivyokuwa kwenye vidole vya mkomunishaji, vya juu ya kiganja, na vidole vya aliye komunika. Katika hostia 25 walipata matokeo haya = vipande 92 vilionekana kwa macho. 27 + 47 + 18 = 92.
Hebu tufikirie tunatupa hostia ngapi? Mara nagapi tunazikanyaga pale mbele tunpokwenda kupokea? Kufuru ya aina gani hiyo? Je, tuendelee hivyo? Je, sisi tunaotupa, tunaokanyaga bila kujali tunatarajia kukumbatiwa na kupongezwa mbinguni na YESU kwa kufuru hiyo?
Mfalme wa Japani katika karnekadhaa zilizopita alipokuwa akiwaua wakatoliki wa kweli kwa ukatili aliwalazima kukana imani yao kwa kukanyaga msalaba wa mbao bila mwili. Japo alikuwa mtu mwovu kiasi hicho, hakuthubutu kuwaambia wakanyage Ekaristi Takatifu. Je, sisi?
Matokeo ya kugawa Ekaristi Takatifu mkononi
· Mtu mmoja alikuwa nazo nyumbani kwake 200 na alizipini ukutani akichora umbo la kipepeo.
· Wengine waliichukua na kuipasua ili waone kama damu itatoka kisha wakatupa chooni.
· Mwingine aliichukua na kuisahau mfukoni hadi ilipooneka Dry cleaner kwenye mfuko wake wa suruali.
· Mwingine walimkuta nazo 17 akiziuza kwa Franck moja kwa kila Ekaristi.
· Miaka kadhaa iliyopita Ekaristi zaidi ya 200 zilikamatwa uwanja wa ndege wa Dar zikisafirishwa nje.
· Mwezi Februari mwaka wa 2007 nilipokea barua ikinionya kuwa watu wanachukua Ekaristi na kwendanazo. Nilithibitisha hili baada ya mwamini mmoja kuniambia kwamba mtu mmoja alichukua Ekaristi na kwenda nayo nyumbani kisha alimwonyesha. Hta mama mmoja kwenye misa ya mchana alionwa na watu akichukua Ekaristi paada ya kupewa na kukimbia nayo mara tu baada ya misa.
Hivyo tujitahidi sana kuepuka kuendelea kupokea kwa mkono. MUNGU siyo shemeji yetu hadi tufikie hatua hiyo.
Tunaagizwa kupokea Ekaristi Takatifu katika hali ya neema. Hiki ni chakula lakini si chakula cha kawaida tu. Kwa kutokujali wengi wanapokea Ekaristi Takatifu bila kuwa katika hali ya neema ya utakaso. Ni kufuru ni sawasawa na kuandaa chakula vizuri na kwenda kukilia chakula hicho chooni. Ni heri usiisogelee Ekaristi Takatifu tusipokuwa katika hali ya neema ya utakaso. MUNGU hawezi kuchezewa na kiumbe awaye yote. Kama vile usivyoweka kidole chako kwenye moto, ukiogopa kuungua vivyo hivyo kwa Mwenyezi MUNGU.
Muujiza wa Lanciano – Italy 700
Mwujiza huu ulitokea kwa padre mmoja wa Shirika la Mt. Basili ambaye alikuwa na mashaka sana na mkate kugeuka kuwa mwili wa YESU na divai kuwa Damu ya YESU. Siku moja akiwa anaadhimisha ibada muujiza huo ulitokea na alijishtukia akipiga kelele; Nyama!!! Damu!!! Wanasayansi walipima na pasipo mashaka walihakikisha kabisa kwamba kweli ilikuwa nyama na damu ya mwanadamu. Hadi leo vipo. Tena ile damu imeganda katika vipande vitano kwa ukubwa na umbo tofauti lakini kila kibonge kimoja uzito wake ni sawa sawa na vyote ukipima kwa pamoja!!!!!!!!!!!!!

Wito ni kwamba tupokee Ekaristi Takatifu tukiwa katika neema ya utakaso na ikiwezekana tukiwa tumepiga magoti mdomoni. Endapo tutakuwa tunapokea tukiwa tumesimama, ni vema tuoneshe ishara ya heshima kwa Ekaristi Takatifu kwa kufunga mikono na kuinama kisha kupokea, au kupiga goti kisha kisimama na kupokea.
Asanteee sanaaa fr kwa maelezo mazuri
ReplyDeleteKupokelea Ekaristi Takatifu mikono kunapelekea Yesu wa Ekaristi tumkanyagekanyage kwani ni vipande (kwa maanan ya Kristo nzima Hata kama ni kipande)vipande VINGI vinadondoka. Wala tusisingizie kuambukizana magonjwa. Hakuna ushahidi wa wazi uliothibitisha kuwa Wakristo wameambukizana magonjwa kwa kumpokelea Yesu wa Ekaristi midomoni.Je ni IMANI HABA unafanya tuone kupokelea mkononi ni sawa? Hakika hadhi ya Yesu Kristo akiwa katika maumbo ya mkate na divai inabidi kuporomoka; tukiendelea hivyo itafika mahali tutakuwa tunafananisha na chakula Cha kawaida.
ReplyDelete